Home Uncategorized NENGA,NANDY WAPEWA KADI NA RAIS

NENGA,NANDY WAPEWA KADI NA RAIS

 RAIS  wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amewakabidhi kadi za uanachama kwa Wasanii Faustina Mfinanga wanamjua kwa jina la Nandy na William Lyimo  wengi wanauita Nenga.

Wawili hao kwa sasa ni mwili mmoja baada ya kukamilisha kufunga pingu za maisha wikiendi hii.

Mbali na kadi hizo pia Injinia Hersi aliwakabidhi fedha  Tsh Mil 5,ikiwa ni pongezi kwa mashabiki hao wa Yanga.

 Rais huyo ambaye amechaguliwa hivi karibuni alikuwa mmoja ya watu maarufu waliohudhuria sherehe  ya mastaa hao wa Bongo Fleva iliyofanyika Mlimami City, Dar es salaam.

Nandy na Billnass wamefunga pingu ya maisha katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach Dar na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki.

Ikawe kheri na baraka kwenu katika hatua nyingine.

Previous articleSIMBA YAFUNGA USAJILI NA MASHINE HIZI TATU,NDANI YA CHAMPION JUMATATU
Next articleBEKI APEWA MKATABA MGUMU AKUBALI KUSAINI JANGWANI