Home Sports MAKOCHA WATATU KUINOA SIMBA

MAKOCHA WATATU KUINOA SIMBA

SIMBA itakuwa na makocha wawili wasaidizi kwa msimu wa 2022/23 baada ya mmoja kuongezwa rasmi na atakuwa na majukumu mawili kwa wakati mmoja kwenye kikosi hicho.

Tayari Kocha Mkuu ameshatangazwa ambaye ni Zoran Maki yupo na kikosi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi kuelekea msimu ujao ambapo alianza kazi na kocha mzawa msaidizi Seleman Matola.

Rasmi sasa kocha mwingine msaidizi atakuwa ni Sbai Karim ambaye atakuwa pia ni kocha wa viungo ndani ya Simba ambaye alitangazwa Julai 16.

Ikumbukwe kwamba Karim anachukua mikoba ya Daniel De Castro aliyekuwa kocha wa viungo wa timu ya Simba lakini alichimbishwa virago mazima.

Nafasi ambayo imebaki kwa sasa ndani ya Simba ni ile ya kocha wa makipa ambaye alikuwa ni Tyron Damos ambaye amepata timu mpya nchini Afrika Kusini.

Hivyo kwenye benchi la ufundi kutakuwa na makocha watatu ambao ni Maki,Matola na Karim.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
Next articleAZAM FC WAMETISHA WATWAA UBINGWA NA BADO WANA MECHI