Home Sports BM:MASHABIKI MSIWE NA MASHAKA MSIMU UTAKUWA MZURI

BM:MASHABIKI MSIWE NA MASHAKA MSIMU UTAKUWA MZURI

KIUNGO mpya wa Yanga, Bernard Morrison amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka msimu mpya utakuwa ni mzuri kwao na watapambana kufanya vizuri.

BM amerejea ndani ya Yanga kwa kupewa dili la miaka miwili baada ya dili lake ndani ya Simba kugota ukingoni.

Nyota huyo amewaambia mashabiki wa Yanga kuwa aliwakosea wakati ule alipokuwa ndani ya Simba lakini wamempokea hivyo itakuwa ni kazi kwake kufanya vizuri kwa kushirikiana na wengine.

“Nimerudi Yanga kwa mara nyingine tena kuna jambo ambalo nitalifanya na nina amini kwamba tutafanya jambo kubwa kwa kila mmoja hakuna ambacho kinashindikana.

“Yale ambayo yalitokea msimu ule uliopita wakati ninaondoka nimeona kwamba mmenipokea vizuri hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya sisi tuna watu tuna watu,’ amesema.

Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022/23 na kambi yao wanatarajiwa kuweza kuiweka Morogoro kwa ajili ya kujifua vema zaidi.

Previous articleKAMBI YA SIMBA MISRI NI NOMA
Next articleSAUTI:KIUNGO MGHANA AMETAMBULISHWA AZAM FC