Home Uncategorized KAMBI YA SIMBA MISRI NI NOMA

KAMBI YA SIMBA MISRI NI NOMA

WASHINDI namba mbili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba wameweza kufika salama nchini Misri baada ya safari yao kuanza jana Julai 14,2022.

Msafara huo umeweka kambi nchini Misri ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 Simba ilikwama kusepa na taji lolote na kuwafanya watani zao wa jadi kuweza kutwaa mataji yote matatu kuanzia Ngao ya Jamii,Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara.

Jana msafara wa Simba ikiwa ni pamoja na nahodha John Bocco,Meddie Kagere na Kocha Mkuu, Zoran Maki raia wa Misri waliweza kukwea pia kuelekea Misri na leo wamefika salama.

Ahmed Ally,Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba amesema kuwa kambi yao ni maalumu kwa ajili ya kuweza kurejea kwenye ubora wao.

“Ukweli ni kwamba tumekwama kutwaa mataji msimu uliopita lakini msimu ujao tunakwenda kufanya kazi ya kurejesha mataji ambayo tuliyapoteza na kambi ipo vizuri,” amesema.

Previous articleSAUTI:BEKI MPYA YANGA LOMALISA AFUNGUKA
Next articleBM:MASHABIKI MSIWE NA MASHAKA MSIMU UTAKUWA MZURI