Home Sports RATIBA YA NGAO YA JAMII YAWEKWA WAZI, LIGI KUANZA AGOSTI 17, 2022

RATIBA YA NGAO YA JAMII YAWEKWA WAZI, LIGI KUANZA AGOSTI 17, 2022

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi TPLB, Almasi Kasongo leo Juni 28, 2022 ametangaza ratiba ya mchezo wa Ngao ya hisani kuwa utachezwa Agosti 13, 2022 mwaka huu.

 

Kasongo amefafanua zaidi kwa kusema kikanuni mchezo huo hukutanisha bingwa wa ligi na bingwa wa FA, lakini iwapo bingwa wa ligi na FA akiwa ni mmoja basi mchezo huo uta wakutanisha mshindi wa ligi na aliyemaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Bodi ya ligi pia imetangaza rasmi kuwa msimu wa 2022/23 unatarajiwa kuanza Agosti 17, 2022  mwaka huu huku ukitarajiwa kumalizika Mei 17 mwaka 2023

Previous articleEXCLUSIVE: DEREVA ALIYEENDESHA BASI LA YANGA LA UBINGWA KUTOKA UGANDA, AFUNGUKA MENGI USIYOYAJUA..
Next articleHIZI HAPA TIMU ZITAKAZOSHIRIKI KIMATAIFA BONGO