Home Sports HIZI HAPA TIMU ZITAKAZOSHIRIKI KIMATAIFA BONGO

HIZI HAPA TIMU ZITAKAZOSHIRIKI KIMATAIFA BONGO

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo amesema kuwa ni timu nne ambazo zitaiwakilisha Tanzania katika anga la kimataifa.

 Ni katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ni nafasi nne zipo kwa timu za Tanzania.

Kasongo amesema Yanga na Simba tayari wameshapatikana kuwakilisha michuano ya Ligi ya Mabingwa kinachosubiriwa ni timu mbili zitakazoenda kuwakilisha Kombe la Shirikisho la Afrika.

“Timu nne zitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ambapo Yanga ambaye ni bingwa pamoja na Simba mshindi wa pili hawa watakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwenye timu hizo ni timu tatu zitatoka kwenye ligi ambazo zitamaliza kwenye nafasi tatu za juu na timu moja ni le itakayotwaa Kombe la Shirikisho.

“Katika Kombe la Shirikisho timu itakayobeba ubingwa itashiriki katika Kombe la Shirikisho ila kama bingwa wa kombe la Shirikisho atakuwa ametwaa ubingwa wa Shirikisho basi timu nne zitatoka kwenye ligi,” amesema.

Pia ratiba ya ligi inatarajiwa kuwekwa wazi kuanzia kesho ambapo mchezo wa Ngao ya Jamii unatarajiwa kuchezwa Agosti 13 Agosti 2022 na mchezo wa kwanza wa ligi unatarajiwa kuchezwa Agosti 17,2022.

Fainali ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kuchezwa Julai 2,kati ya Yanga v Coastal Union.

Previous articleRATIBA YA NGAO YA JAMII YAWEKWA WAZI, LIGI KUANZA AGOSTI 17, 2022
Next articleKOCHA HUYU ATAJWA KUINGIA ANGA ZA SIMBA