Home Sports KUMBE YANGA WALIPANIA KITAMBO KWELI

KUMBE YANGA WALIPANIA KITAMBO KWELI

YANGA jana Jumapili waliweza kulisimamisha Jiji la Dar wakiwa wanalitembeza kombe lao la Ligi Kuu Bara walilolitwaa msimu huu wa 2021/22.

 Ubingwa huo ni wa 28 kwa Yanga ambapo jana Jumamosi walikabidhiwa kombe lao baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 Msemaji wa Yanga, Haji Manara, mapema kabisa alibainisha kwamba watafanya jambo kubwa na kuweka rekodi ya kupokea taji hilo la ligi kwa msimu wa 2021/22.

 “Kitu cha muhimu zaidi kwa Wanayanga ni kuhakikisha wanakuja Uwanja wa Ndege Dar kuwapokea wachezaji na makocha wakiwa na kombe wakitokea Mbeya, kisha tulitembeze kombe hilo jiji zima na kuwaonesha watu ni namna gani Yanga hatuna jambo dogo.

 “Mitaa ambao tutapita ni Msimbazi, Posta, Jangwani na sehemu nyingine nyingi ili tuhakikishe kuwa kila Mwanayanga wa Dar anafurahia mafanikio ya timu yake, kumbuka pia kuna ubwabwa pale makao makuu ya klabu, baadaye tutaenda kufanya sherehe ambayo tutawatangazia.”.

Jana Yanga waliweza kufanya jambo lao baada ya kulipokea kombe hilo na ilikuwa ni furaha kwa kila shabiki wa Yanga pamoja na wachezaji walioweza kutimiza majukumu yao.

Previous articleKIUNGO WA KAZI SIMBA APEWA MKATABA
Next articleKOCHA WA MANULA APATA DILI AFRIKA KUSINI