MAMBO MAKUBWA MAWILI YA KUFANYA KWA SASA

    MAMBO makubwa mawili kwa sasa yapo kwenye hesabu za kila mmoja,mwisho wa msimu pamoja na mwanzo wa msimu mpya.

    Haya lazima yaweze kuzunguka kwenye familia ya mpira hasa ukizingatia kwamba muhimu kila mmoja kufanya yale ambayo yanamuhusu kutimiza.

    Ukweli ni kwamba kila timu iwe ni ya ligi pamoja na zile ambazo zilikuwa kwenye Championship zina hesabu ambazo zilihitaji kuzifanya.

    Zipo ambazo ziliweza kutimiza na zipo ambazo zinapambana kuendelea kutimiza majukumu hayo hivyo muhimu ni kuangalia mwisho utakuwa kwa namna gani.

    Ikiwa mambo bado ni magumu kwa Championship kwenye kutimiza majukumu yao ni muda wa kupanga mpango kazi mpya kwa wakati ujao.

    Maisha ya mpira yanaishi kila siku na kila wakati ni muda wa maboresho kwa pale ambapo timu inakwama kupata kile ambacho ilikuwa inahitaji.

    Yote kwa yote zipo ambazo zimepanda ndani ya ligi hapa kazi zao ni kuweza kujipanga upya kwa msimu mpya kwa kuwa wanaanza maisha mapya.

    Nyingine zipo zinaishi ndani ya Championship hizi nazo malengo yao ni kuona zinaweza kuibuka kwenye ligi kuu msimu mwingine kwa kuwa kwa sasa hesabu zimewagomea.

    Lakini kama zipo ambazo zilikuwa zinahitaji kubaki ndani ya Championship na zikabaki basi hilo sio jambo baya kwa kuwa malengo yao yametimia hivyo wana kazi ya kupanga mpango kazi mpya.

    Kwa upande wa Ligi ya Wanawake Tanzania tumeona kwamba kila msimu unakuwa tofauti huku ushindani ukiwa ni mkubwa kila wakati.

    Hapa pia zile ambazo zilikuwa zinapambana kuweza kuwa ndani ya tano bora kama zilikwama basi ni muda wa kutazama wapi waliweza kushindwa.

    Ipo wazi kuwa suala la uwekezaji hasa kwa wadhamini upande huu wengi wanaangalia pembeni hivyo kwa msimu ujao itapendeza wawekezaji pia wakitazama namna ya kuweza kuuinua mpira wetu.

    Hawa wasichana wamekuwa wakitutoa kimasomaso kwenye mechi za kimataifa na hili linatufanya tuweze kuwa na deni kwao hasa katika kuhakikisha wanakuwa wakifanya kazi kwenye mazingira imara.

    Kufanya kwao vizuri kimataifa iwe ni chachu kwetu kuongeza nguvu kwenye uwekezaji na kuwapa nguvu ya kuweza kuwa imara kwa wakati ujao.

    Tukirudi kwenye ligi kuu hapa napo zipo ambazo zitashuka kwa kuwa hili haliepukiki lazima liwepo hivyo kinachopaswa sio muda wa kuanza kulaumiana bali kuweza kutazama anguko lilikuwa wapi.

    Ikiwa timu itatambua pale ambapo ilikwama basi ina nguvu ya kuweza kuongeza nguvu kwa wakati ujao na kufanya kazi kwa umakini kupata matokeo mazuri.

    Muda wa kujipanga ni sasa na hapa ni wakati sahihi hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji kuweza kuwa ndani ya ligi lakini sharti mbili zishuke jumlajumla na mbili zitacheza mchezo wa mtoano.

    Zenye nafasi ya kucheza mtoano bado zina nafasi ya kujinasua hapo zilipo kwa kusaka ushindi kwenye mechi zijazo na zilizobaki kwa kuwa ligi haijaisha.

    Zile ambazo zipo kwenye nafasi ya kushuka daraja nazo pia zinaweza kujinasua hapo na kuwa kwenye nafasi ya mtoano kikubwa ni maandalizi.

    Kwa zile ambazo zimeweza kufikia malengo yao pongezi na ziwe juu yao na kwa zile ambazo zimeshindwa kufikia malengo ni lazima kutazama pale ambapo walikosea ili waweze kupata matokeo wakati ujao.

    Previous articleBWALYA AWEKA WAZI KWAMBA AMEJIFUNZA MENGI SIMBA
    Next articleNAMNA MAYELE ALIVYOIVUNJA REKODI YA BOCCO