Home Sports NAMNA MAYELE ALIVYOIVUNJA REKODI YA BOCCO

NAMNA MAYELE ALIVYOIVUNJA REKODI YA BOCCO

FISTON Mayele, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga amevunja rekodi ya staa wa Simba, John Bocco kwenye suala la ufungaji na pasi za mabao.

Bocco msimu wa 2020/21 aliweza kutupia mabao 16 na pasi mbili na aliweza kuibuka mfungaji bora ambaye anatetea kiatu chake hicho.

Msimu huu Bocco kafunga mabao matatu na hajatoa pasi ya bao huku rekodi yake ikivunjwa na Mayele ambaye ametupia mabao 16 na pasi nne za mabao.

Mayele aliifikia rekodi ya Bocco,kwenye mchezo wa ligi uliochezwa dhidi ya Coastal Union ambapo aliweza kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao kwa Chico Ushindi wakati Yanga walipotangazwa kuwa mabingwa wa ligi msimu wa 2021/22.

Mayele amesema kuwa bado anaamini kazi inaendelea katika kutimiza majukumu yake kwenye mechi ambazo zimebaki.

“Bado kuna mechi za kucheza hivyo kazi kubwa ni kuweza kutimiza majukumu yangu nikipata nafasi nitafunga ama kutengeneza nafasi,”.

Previous articleMAMBO MAKUBWA MAWILI YA KUFANYA KWA SASA
Next articleKOCHA AFUNGUKIA KASI YA MPOLE