Home Sports NBC YATAMBULISHA KOMBE JIPYA LA LIGI KUU BARA

NBC YATAMBULISHA KOMBE JIPYA LA LIGI KUU BARA

 MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo ametambulisha Kombe Jipya atakalopewa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2021/2022.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Kasongo amewashukuru wanahabari na wadau wote wa mpira kwa michango yao katika kukuza soka la nchi hii, lakini pia namna ambavyo wanauongelea mpira wa nchi pamoja na changamoto walizonazo Bodi ya Ligi ambazo yeye Mtendaji Mkuu anaridhika nazo na anazifanyia kazi kwa kuwa changamoto ni fursa.

Kasongo pia ameongeza kuwa Bodi ya Ligi kwa kushirikiana na TFF imejipanga kufanya mambo kisasa kwani ina mpango wa kuandaa Replica au mfanano wa Kombe halisi la Mshindi wa Ligi Kuu ya NBC ili pale inapotokea hatua kuwa hadi siku ya mwisho Bingwa anakuwa hajafahamika basi Replica hizo zinasambaa katika Viwanja husika ambavyo ikitokea Bingwa akapatikana basi anakabidhiwa Kombe lake mara moja.

Aidha Kasongo amewashukuru na kuwapongeza wadhamini mbalimbali wa soka nchini wakiwemo NBC, Azam Media na wengineo kwa mchango wake katika kuiheshimisha Ligi Kuu nchini kwani hadi sasa Ligi Kuu ikiwa katika raundi ya 24 haijulikani timu gani imeshuka daraja, timu gani imejihakikishia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini.

Previous articleMAKOCHA 100 WAOMBA KAZI SIMBA
Next articleINJINIA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS