Home Sports INJINIA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

INJINIA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS

JUNI 9,2022, Injinia Hersi Said amerejesha fomu yake ya kugombea Urais wa Yanga kupitia wawakilishi wake.

Injinia amewakilishwa na wazee wa Yanga pamoja na Fredrick Mwakalebela ambaye rasmi amesema kuwa yeye hatogombea na kuwaaga wana Yanga kwenye nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injini Hersi jana alichukuliwa fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Julai na wazee wa klabu hiyo.

Leo wazee wa Klabu ya Yanga wamerudisha fomu hiyo ikiwa imejazwa tayari kwa kuanza mbio za Urais wa Klabu hiyo.

Mwakalebela amesema kuwa Yanga wanatambua namna Injinia alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya timu.

“Wote najua kwamba mnajua juhudi za Injinia kila mechi ilipokuwa inachezwa yeye alikuwepo,hivyo mimi ninamuunga mkono kwa asilimia 100,”.

Sababu ya Injinia kushindwa kurejesha fomu ni ratiba kushindwa kuwa rafiki kwake jambo lililofanya aweze kurejeshewa.

Previous articleNBC YATAMBULISHA KOMBE JIPYA LA LIGI KUU BARA
Next articleLACAZETTE NI MALI YA LYON