Home Sports MAKOCHA 100 WAOMBA KAZI SIMBA

MAKOCHA 100 WAOMBA KAZI SIMBA

INATAJWA kwamba makocha zaidi ya 100 wametuma CV zao kwa ajili ya kuoma dili la kuifundisha Klabu ya Simba.

Simba kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha, Seleman Matola ambaye anafanya kazi ya kusimamia mipango ya timu hiyo.

Alikuwa ni Pablo Franco ambaye amefutwa kazi Mei 31 kutokana na kushindwa kutimiza malengo ya Simba.

Habari zimeeleza kwamba zaidi ya makocha 100 kutoka sehemu mbalimbali wameomba kupata tenda ya kuinoa Simba yenye nyota kama Meddie Kagere na Kibu Dennis.

“Kuna zaidi ya CV 100 kutoka kwa makocha tofauti ambao wanahitaji kuweza kuifundisha Sima hivyo ni suala la kusubiri,” ilieleza taarifa hiyo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuwa wapo makocha ambao wametuma CV zao hivyo wakati ukifika kocha mpya atatambulishwa.

Previous articleBANDA AINGIA ANGA ZA YANGA
Next articleNBC YATAMBULISHA KOMBE JIPYA LA LIGI KUU BARA