Home Sports UBAGUZI WA RANGI WAITESA ENGLAND

UBAGUZI WA RANGI WAITESA ENGLAND

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amekiri kuwa kwenye mtego wa kupata ugumu wa kuchagua wapigaji wa penalti kwenye kikosi chake kutokana na hofu kubwa ya baadhi ya nyota wa kikosi hicho kukumbana na masuala ya ubaguzi wa rangi.

Bukayo Saka, Marcus Rashford na Jadon Sancho wote walifanyiwa ubaguzi mbaya mtandaoni baada ya kukosa penalti zao katika mechi ya fainali ya michuano ya Euro 2020 dhidi ya Italia, huku Southgate akikiri kukasirishwa na matukio hayo.

Bosi huyo wa England alisema: “Lazima niseme kwamba haikuwahi kuingia akilini mwangu hapo mwanzo, sasa najua tutakutana na wakati mgumu katika kufanya uchaguzi wa nani watapiga penalti kwa kuwa wengi wao wanaweza kuwa na hofu na masuala ya ubaguzi wa rangi.

“Lakini haitakuwa sawa kutochagua wachezaji unaofikiri kuwa ni bora kuwachukua kwa sababu tu wanaweza kukosa na kukutana na changamoto hiyo, lazima niwachague kwa imani kwamba watafunga, tuna watu kama Harry Kane, Reece James, Trent na Saka wameonekana kuwa bora katika eneo hilo.”

Previous articleMAN CITY KUMNG’OA SAKA ARSENAL
Next articleBAYERN WAZIDI KUMKOMALIA MANE