Home Sports BAYERN WAZIDI KUMKOMALIA MANE

BAYERN WAZIDI KUMKOMALIA MANE

BAYERN Munich wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pili ya dau la pauni milioni 30, kwa ajili ya kukamilisha usajili wa staa wa kimataifa wa Liverpool raia wa Senegal, Sadio Mane mara baada ya Liverpool kukataa ofa ya kwanza na sasa wanataka pauni milioni 42.5.

Sportsmail limeripoti kuwa Liverpool ilitupilia mbali ofa ya kwanza ya Bayern ya pauni milioni 21 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 4.6 kama Wajerumani hao wangefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Liverpool wanataka karibu pauni milioni 42.5 kwa Mane, 30, wakiwa wanamtazama mshambuliaji wa Benfica, Darwin Nunez kama mbadala wake.

Mane amebakiza miezi 12 kukamilisha mkataba wake wa sasa na amedokeza kwamba mustakabali wake unaweza kuwa mahali pengine.

Lakini Sportsmail ilifichua kwamba Mane tayari amemuuliza mchezaji mwenzake wa Liverpool, Thiago kama anaweza kuhamia kwenye nyumba yake mjini Munich ikiwa atajiunga na Bayern msimu huu wa joto.

Rais wa Bayern, Herbert Hainer akizungumzia uwezekano wa kumnunua Mane, aliliambia jarida la Ujerumani BILD akisema: “Ikiwa tunataka mchezaji kweli, tunaweza kumpata. Lakini anapaswa kutufaa.”

Previous articleUBAGUZI WA RANGI WAITESA ENGLAND
Next articleTANZANIA YAPOTEZA MBELE YA ALGERIA