Home Sports TANZANIA YAPOTEZA MBELE YA ALGERIA

TANZANIA YAPOTEZA MBELE YA ALGERIA

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu,Kim Poulsen leo Juni 8,2022  imeambulia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Algeria katika mechi ya pili ya kufuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika AFCON zinazotarajiwa kufanyika 2023 nchini Ivory Coast.

Ndani ya dk 40 Stars iliweza kujilinda lakini makosa katika dk ya 45 liliweza kuwapa nafasi Algeria kupachika bao la kuongoza muda mfupi kabla ya mapumziko kwa bao la Amir Selmane.

Kipindi cha pili Poulsen aliweza kufanya mabadiliko kwa  kuwaingiza Kibu Dennis, George Mpole, Kelvin John na Salum Abubakar huku waliotoka ikiwa ni Feisal Salum,Simon Msuva,Nickosn Kibabage na Novatus Dismas.

 Wakati Stars ikiwa na matumaini ya kupata bao la kuweka mzani sawa dk ya 89, waliweza kufungwa kwa shambulizi la kushtukiza kupitia kwa Mohamed El Amine ambaye alianzia benchi.

Poulsen aliweka wazi kwamba kulikuwa na ugumu wa kuweza kupambana na wachezaji bora na imara hivyo ni moja ya somo ambalo watalifanyia kazi.

Previous articleBAYERN WAZIDI KUMKOMALIA MANE
Next articleBIASHARA UNITED YAPATA KOCHA MPYA