Home Sports BIASHARA UNITED YAPATA KOCHA MPYA

BIASHARA UNITED YAPATA KOCHA MPYA

UONGOZI wa Biashara United umetangaza benchi jipya la ufundi kwa ajili ya kumaliza mechi nne za msimu 2021/22.

 Ni Vivier Bahati ambaye alikuwa kocha mkuu, msaidizi wake Daddy Gilbert na meneja Frank Wabale hawa wote wamefutwa kazi.

Kocha Mkuu ni Khalid Adam atakuwa kocha Mkuu wa Biashara United ambayo inapambana kushuka daraja kwa sasa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Biashara United, Sakma Thabit amesema kuwa ni Khalid Adam atakuwa kocha mkuu,Omari Madenge atakuwa msaidizi na Omari Hamis akiwa ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Timu hiyo kwenye mechi sita za ligi ilikusanya pointi mbili ambapo mchezo wa mwisho ilikuwa ni kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Previous articleTANZANIA YAPOTEZA MBELE YA ALGERIA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI