Home Sports MAN CITY KUMNG’OA SAKA ARSENAL

MAN CITY KUMNG’OA SAKA ARSENAL

Manchester, England

MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester City wametajwa kuwa wanafuatilia kwa karibu mustakabali wa staa wa Arsenal, Bukayo Saka katika kipindi cha miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake ili kuona uwezekano wa kumng’oa mchezaji huyo kutoka Emirates.

Inaelezwa kuwa City pamoja na wapinzani wao wakubwa Liverpool wote wanamtazama staa huyo wa Arsenal kama mbadala sahihi wa baadaye wakati huu ambapo Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumpa mkataba mrefu.

Mkataba wa sasa wa Saka una kipengele cha kumfanya aendelee kusalia Arsenal mpaka mwaka 2024 huku ukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine ambapo tayari majadiliano ya awali yalikuwa yamefanyika kuelekea mwisho wa msimu na Arsenal hawataki kuruhusu kandarasi ya Saka kufikia ukingoni.

Hata hivyo, kushindwa kwa Arsenal kufuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumeongeza matumaini ya Liverpool na City kumng’oa Saka Arsenal.

Ubaguzi wa rangi waitesa England London, Uingereza

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amekiri kuwa kwenye mtego wa kupata ugumu wa kuchagua wapigaji wa penalti kwenye kikosi chake kutokana na hofu kubwa ya baadhi ya nyota wa kikosi hicho kukumbana na masuala ya ubaguzi wa rangi.

Previous articleVIDEO: MCHAMBUZI EDGA KIBWANA AWACHAMBUA MSUVA, SAMATTA KATIKA KIKOSI CHA STARS
Next articleUBAGUZI WA RANGI WAITESA ENGLAND