Home Sports LEBRON JAMES AWA MCHEZAJI WA KWANZA BILIONEA AKICHEZA LIGI YA NBA

LEBRON JAMES AWA MCHEZAJI WA KWANZA BILIONEA AKICHEZA LIGI YA NBA

LeBron James– Nyota mara 18 wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA na bingwa mara 4 wa NBA, mbali na kuwa mshindi wa medali ya dhahabu mara 2 kwenye Olimpiki – amepiga hatua nyingine muhimu, wakati huu akifanya kitu ambacho hakuna mchezaji mwingine wa NBA amewahi kufanya.

Baada ya mwaka mwingine mbaya wa mapato– ya jumla ya dola milioni 121.2 mwaka jana–Forbes inakadiria kuwa James amekuwa bilionea rasmi, huku akiendelea kushiriki katika mchezo huo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 ana utajiri wa dola bilioni 1, kulingana na hesabu ya Forbes. James, ambaye amekosa mechi za mchujo kwa mara ya nne pekee katika misimu wake wa 19, ndiye mchezaji wa kwanza wa NBA aliye hai kuingia katika orodha ya mabilionea.

(Michael Jordan, bilionea mwingine pekee wa mpira wa vikapu, hakufikia ubilionea hadi 2014 – zaidi ya muongo mmoja baada ya kustaafu, kufuatia hatua yake ya kuwekeza katika timu ya mpira wa vikapu ya Charlotte Hornets.)

Previous articleTHIAGO AAMBIWA KWAMBA HAMNA KITU
Next articleMKALI WA PASI NDANI YA SIMBA KUTIMKIA AFRIKA KUSINI