Home Sports MKALI WA PASI NDANI YA SIMBA KUTIMKIA AFRIKA KUSINI

MKALI WA PASI NDANI YA SIMBA KUTIMKIA AFRIKA KUSINI

IMEELEZWA kuwa kiungo namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya Simba msimu wa 2021/22 Rally Bwalya yupo kwenye hesabu za timu moja ya Afrika Kusini.
Inatajwa kwamba ni Klabu ya Amazulu ya Afrika Kusini inahitaji saini ya raia huyo wa Zambia kwa ajili ya msimu ujao.

Ikumbukwe kwamba kiungo huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu ya Power Dynamo ya Zambia na kusaini dili la miaka mitatu.

Kabakisha mwaka mmoja ndani ya Simba ambao utanunuliwa na timu hiyo ambayo inahitaji saini yake.

Kwenye ligi katoa pasi 3 za mabao na kufunga bao moja kati ya mabao 33.

Kuhusu masuala ya usajili,hivi karibuni Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kila kitu kitatolewa taarifa wakati ukifika

Previous articleLEBRON JAMES AWA MCHEZAJI WA KWANZA BILIONEA AKICHEZA LIGI YA NBA
Next articleKUNA WINGA YANGA ALITISHIWA KUROGWA