Home Sports THIAGO AAMBIWA KWAMBA HAMNA KITU

THIAGO AAMBIWA KWAMBA HAMNA KITU

GWIJI wa Liverpool, Dietmar Hamann amemshukia kiungo Thiago Alcantra akiweka wazi kuwa ni moja ya wachezaji wa Ulaya wanaopewa sifa kubwa tofauti na uwezo wake.

Mjerumani huyo amesema Thiago ni bure kabisa timu napokuwa haina mpira licha ya kwamba amesifiwa alikuwa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Jurgen Klopp.

Nyota huyo ni miongoni mwa wale ambao walitwaa makombe mawili ilikuwa ni lile la FA na Kombe la Ligi ila Hamann sio shabiki wa nyota huyo.

“Sielewi sifa nyingi kupita kiasi kwa Thiago zinatokea wapi, kwanu mimi huyu ni mmoja ya wachezaji wa Ulaya wanaopewa sifa nyingi mno tofauti na uwezo wao,” amesema.

Previous articleVIDEO: MAMBO NI MOTO YANGA, WATANGAZA UCHAGUZI MKUU KUMPATA RAIS NA MAKAMU WAKE
Next articleLEBRON JAMES AWA MCHEZAJI WA KWANZA BILIONEA AKICHEZA LIGI YA NBA