Home Sports JUMA MGUNDA NA KASI YAKE MEI NI MOTO

JUMA MGUNDA NA KASI YAKE MEI NI MOTO

KASI ya Coastal Union ndani ya Mei inafurahisha kwa kuwa kwenye mechi 5 ambazo wamecheza hawajapoteza mchezo wakishinda nne na kuambulia sare moja ugenini.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa watu wasijisahaulishe wanapaswa kuiombea timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri.

“Tupo nafasi ya 6 wazidi kutuombea ili kwenye mechi zijazo tupate matokeo na msimu ujao tuzidi kuwepo kwenye ligi,” alisema.

Kutokana na kasi hiyo tuzo ya kocha bora pamoja na mchezaji aliyefanya vizuri ndani ya Mei ipo kwa Mgunda pamoja na kijana wake Abdul Seleman, ‘Sopu’ kwa kuwa kwenye mabao matano ambayo yamefungwa na timu hiyo yeye katupia matatu.

Mwendo wa Coastal Union ulikuwa namna hii:- Mei 24,2022 Mbeya Kwanza 0-1 Coastal Union, Uwanja wa Sokoine,Mei 20, Coastal Union 2-1 Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkwakwani.

Mei 15,Mtibwa Sugar 0-0 Coastal Union, Uwanja wa Manungu,Mei 11, Coastal Union 1-0 Biashara United, Uwanja wa Mkwakwani na Mei 8 ilikuwa Coastal Union 1-0 Polisi Tanzania na kipa namba mbili alikaa langoni kwenye mechi hizo tano anaitwa Mohamed Hussein hajafungwa kwenye mechi 4.

Jana Juni 2 Mgunda na Sopu walitangazwa kutwaa tuzo hizo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Previous articlePOLISI TANZANIA KUWEKA KAMBI DAR
Next articleHOROYA AC, RAJA CASABLANCA ZAMGOMBEA PABLO