Home Sports POLISI TANZANIA KUWEKA KAMBI DAR

POLISI TANZANIA KUWEKA KAMBI DAR

KUTOKANA na kuwa na malengo ya kuhitaji kumaliza ndani ya nne bora, mabosi wa Polisi Tanzania wanafikiria kuweka kambi Dar ili kuweza kufanya maandalizi kwa mechi zilizobaki.

 Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa watapambana kuwashusha waliopo juu yao kwa kutoka chini hivyo watafanya kazi kubwa kwenye mechi zilizobaki.

“Baada ya mchezo wetu dhidi ya Biashara United na kushinda kisha tukatoka hapa maeneo yay a chini tuiyokuwa sasa tunakwenda kuwavutia kasi Namungo na tunaweza kuweka kambi Dar.

“Tunasubiri kuona benchi la ufundi pamoja na kamati namna gani inaweza kutuambia kwamba wapi tuweke kambi hasa ukizingatia kutakuwa na muda wa mapumziko kwa muda hilo litatufanya tuweze kujua muda gani tutapumzika na lini tutaanza maandalizi yetu,” alisema Juma.

Kwenye msimamo Polisi Tanzania ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 26.

Previous articleORODHA YA MASTAA 14 WATAKAOPIGWA PANGA YANGA
Next articleJUMA MGUNDA NA KASI YAKE MEI NI MOTO