Home Sports PARIMATCH YAZINDUA PROMOSHENI YA TWENZETU DUBAI, ZAYLISSA, KIREDIO WAULA

PARIMATCH YAZINDUA PROMOSHENI YA TWENZETU DUBAI, ZAYLISSA, KIREDIO WAULA

 MASHABIKI wa soka, tenisi, UFC, Kriketi, baseball na michezo mingine sasa wanaweza kushinda tiketi ya kwenda Dubai kwa kubashiri na kampuni ya Parimatch Tanzania.

Pia kampuni hiyo imeingia mkataba na muigizaji nyota, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa balozi wa chapa yao, “Brand Ambassodor”.

Mbali ya Zaylissa, pia mchekeshaji maarufu nchini, Vincent Njau “Kiredio” naye ametangazwa kuwa balozi   chapa wa Parimatch wakiungana na meneja wa Habari wa zamani wa Yanga, Haji Manara.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa Parimatch, Levis Paul, jumla ya mashabiki nane (8) watashinda tiketi hiyo kupitia promosheni hiyo ya Twenzetu Dubai na Parimatch ambayo imezinduliwa kwenye hotel ya Serena.

Paul amesema kuwa kutakuwa na droo ya kutangaza washindi kila Alhamis na dhumuni kubwa la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kufurahia ushindi.

Amesema kuwa mbali ya zawadi ya kwenda Dubai, pia kutakuwa na bonasi ya Sh 5,000 kwa yeyote atakayejisajili na Parimatch na kucheza mchezo pendwa wa Aviator.

“Promosheni hiii ni mahususi kwa wateja wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi kipindi hiki. Lengo la kampeni hii ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe za falme za kiarabu huko Dubai.

“Kuanzia Aprili 29 mpaka Juni 30, mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wa Aviator ndani ya Parimatch Casino kupitia tovuti yetu www.parimatch.co.tz au App yetu na kadri unavyoweka beti zaidi ndivyo unajiongezea nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda Dubai au kujishindia bonasi ya Sh5,000 kila siku,” amesema Levis.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya asilimia 125 hadi kufikia Sh 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao.

Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo.

Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.

Wakati huo huo, Zaylissa amesema amefarijika sana kuwa balozi wa Parimatch na atafanya kazi hiyo kwa bidii zote ili kuleta tija katika kampuni hiyo.

“Nawaomba mashabiki zangu wajiunge na Parimatch , kubashiri na kushinda ili kupata nafasi kwenda Dubai,” amesema Zaylissa.

Previous articleAUCHO ATUMA UJUMBE HUU
Next articleYANGA YAFUNGIWA NA FIFA KUSAJILI, KISA HIKI HAPA