DTB NA IHEFU HONGERENI,LALA SALAMA INAHITAJI UMAKINI

    HONGERA kwa DTB pamoja na Ihefu baada ya kuweza kukata tiketi ya kupanda Ligi Kuu Bara hivyo maisha yao ndani ya Championship kwa sasa yamefika mwisho.

    Mwisho wa Championship kwao haina maana kwamba kazi imekwisha ni hatua moja wamepiga hivyo wana kazi kubwa kwa ajili ya msimu ujao kwenye ligi.

    Ambacho kinatokea ni kwamba zipo ambazo zinapanda na zipo ambazo zinashuka haya ni maisha ya kwenye mpira kila siku kila wakati ambacho kinahitajika ni ushindani wa kweli.

    Kila mmoja amevuna kile ambacho alipanda kuanzania mwanzo kwenye maisha ya Championship na ambacho kimepatikana basi mnastahili.

    Ikiwa kuna ambao walipata matokeo ambayo walikuwa hawastahili basi ni wakati mwingine wa kuweza kuangalia namna bora ya kufanya kwa wakati ujao.

    Mashabiki bado mnastahili kupewa pongezi kwa kuwa mlikuwa bega kwa began a DTB pamoja na timu zote ambazo zinashiriki Championship.

    Makosa ambayo yamefanyika ndani ya Championship ni wakati wake kuweza kuyatazama kwa wakati huu ili wakati ujao ushindani uzidi kuwa mkubwa.

    Ugumu mkubwa ulikuwa kwenye masuala ya usimamiaji na mapato kwa timu hizi zinazoshiriki uwa chini huku gharama za uendeshaji zikiwa kubwa.

    Kwenye familia ya michezo ambacho kinadumu na kinapewa kipaumbele kikubwa ni kuzidi kupambana kwa ajili ya kuweza kutatua matatizo haya ambayo kuyamaliza kabisa inaweza kuwa kazi kubwa.

    Kwa upande wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Wanawake tumeona kwamba ushindani mkubwa upon a umeweza kufanya kila mmoja kupata anachostahili.

    Upande wa Ligi ya Wanawake kazi imekwishwa kwenye msako wa bingwa kwa kuwa Simba Queens wameweza kufanikisha lengo hilo hivyo wametetea ubingwa wao wanastahili pongezi.

    Kwa mechi hizi za lala salama basi ni muhimu kila mchezaji pamoja na mashabiki kuweza kujitokeza uwanjani ili kuzipa nguvu timu katika kusaka matokeo.

    Ili uweze kushinda unahitaji kuwa na mashabiki pamoja na wachezaji wazuri ambao watakupa matokeo ambayo unayahitaji kwa wakati.

    Kwa wachezaji kazi yao iwe ni kuwapa furaha mashabiki ambao wanajitoa kwa hali na mali kwa ajili ya timu kupata ushindi.

    Umakini unahitajika katika matumizi ya nafasi pamoja na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi hii itawapa matokeo ya kile ambacho mnahitaji uwanjani.

    Kwa kuwa bado ligi inaendelea basi ni muhimu kila mmoja akatimiza majukumu na kufanya kazi bila kuhofia akifuata zile sheria zizizopo.

    Mashabiki ni wakati wenu kuwa kwenye mwendelezo wa kushangilia timu zenu bila kuchoka kwa kuwa mashabiki wana nguvu kubwa na wakati huu ni ule wa lala salama.

    Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
    Next articleYANGA:SIMBA WALIJIPOTEZEA UBINGWA WENYEWE