Home Sports YANGA:SIMBA WALIJIPOTEZEA UBINGWA WENYEWE

YANGA:SIMBA WALIJIPOTEZEA UBINGWA WENYEWE

MWINYI Zahera,Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana ndani ya Yanga amesema kuwa Simba wamejipotezea ubingwa wa ligi weyewe baada ya kushindwa kuwafunga vinara wa ligi.

Ni Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 24 waliweza kufikisha pointi hizo baada ya ushindi mbele ya Dodoma Jiji kwa mabao 2-0 Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Zahera amesema kuwa nafasi pekee kwa Simba kuweza kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa ilikuwa ni kuwafunga Yanga kwenye mchezo wao wa dabi hapo wengeongeza matumaini ila kupata sare imekuwa kazi kwao.

“Walikuwa na nafasi ya kuweza kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa na walitakiwa kuweza kuifunga Yanga lakini wameshindwa hapo matumaini ya kuweza kutwaa ubingwa wamepoteza.

“Kwa sababu kama wangepunguza pointi zikawa 7 hizo unaweza kusema zinaweza kufikiwa lakini sasa wameachwa kwa zaidi ya pointi 10 unafikiri hiyo ni kazi ndogo.

“Hizo ni mechi 4 ambazo Yanga anapaswa kufungwa tena mfululizo, inawezekanaje jambo hili likatokea?Ila kama likitokea Simba anapaswa kushinda mechi zake zote wewe unadhani inawezekana?

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 49 imecheza mechi 23.

Previous articleDTB NA IHEFU HONGERENI,LALA SALAMA INAHITAJI UMAKINI
Next articleSAUTI:YANGA YASHUSHA MBADALA WA FEI TOTO