LIVERPOOL YAKAA KILELENI KWA MUDA LIGI KUU ENGLAND

LIVERPOOL walikaa kwa muda nafasi ya kwanza kabla ya Manchester City kurejea tena katika nafasi yao walipoweza kushinda mbele ya Leeds United kwa mabao 4-0.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa St James wakiwa ugenini Liverpool ilishinda bao 1-0 dhidi ya Newcastle United

Ni Nabt Keita alipachika bao hilo dk ya 19 akitumia pasi ya Diogo Jota na lilidumu mpaka muda wa mwamuzi kukamilisha dk 90 mchezo wa Ligi Kuu England.

Kipa wa Liverpool, Alison Becker aliweka rekodi ya kufikisha clean sheet 20 akiwa amecheza jumla ya mechi 32 kati ya 34 ambazo timu hiyo imecheza.

Liverpool inafikisha pointi 82 huku City ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 83 zote zimecheza mechi 34.