SIMBA KUTUA BONGO LEO WAKITOKEA AFRIKA KUSINI

BAADA ya kupoteza mbele ya Orlando Pirates wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika leo Aprili 25 wanarejea.

Ni jana Aprili 24 ulipigwa mpira wa kazi na dk 45 Simba walikuwa imara katika eneo la ulinzi huku lile la ushambuliaji ikiwa ni hafifu kwa kuwa walikuwa wakitengeneza mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 58 alipoonyeshwa kadi ya pili Chris Mugalu na kutolewa kwa kadi nyekundu iliwapoteza kwenye ramani Simba na wapinzani wao Orlando Pirates walitumia nafasi moja kuwaadhibu.

Ilikuwa ni dk ya 60 ilitosha kuwapa bao la uongozi Orlando Pirates na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na hatma ya timu inayotinga hatua ya nusu fainali iliamuliwa kwa penalti.

Kila timu imeshinda bao mojamoja katika ardhi ya nyumbani kwa kuwa Simba ilishinda bao moja Uwanja wa Mkapa katika robo fainali ya kwanza.

Orlando Pirates 4-3 Simba, maharamia wanasonga hatua ya nusu fainali, Simba wanarudi Tanzania kuendelea na mbio za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho saa 2:00 usiku wanatarajiwa kuwasili Tanzania.