Home Sports MBADALA WA KANOUTE NA ONYANGO NI HAWA

MBADALA WA KANOUTE NA ONYANGO NI HAWA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ni Sadio Kanoute na Joash Onyango hawa wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Orlando Pirates,Uwanja wa Mkapa.

Ahmed Ally Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanaamini wachezaji hao ni muhimu lakini hakuna namna watawakosa ila wapo wachezaji wengine watakaocheza.

“Tutamkosa Sadio kwa kuwa huyu ana kadi za njano lakini yupo Mzamiru Yassin,Taddeo Lwanga na Jonas Mkude wanaweza kucheza kwenye nafasi yake.

“Pia kwa upande wa Onyango kuna Kennedy Juma pamoja na Pascal Wawa wote ni wachezaji wa Simba wanafanya kazi kwa umakini kutimiza majukumu yao,”.

Mchezaji mwingine wa Simba ambaye atakosa mchezo wa leo unaotarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ni pamoja na Hassan Dilunga ambaye amekwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Nyota huyo aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu,Moro.

Previous articleYANGA WAITAJA TIMU WATAKAYOSHANGILIA UWANJA WA MKAPA
Next articleMANCHESTER UNITED NDANI YA TANO BORA