Home Sports YANGA WAITAJA TIMU WATAKAYOSHANGILIA UWANJA WA MKAPA

YANGA WAITAJA TIMU WATAKAYOSHANGILIA UWANJA WA MKAPA

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umesema leo Jumapili utakuwepo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kwa ajili ya kuisapoti Simba itakapokuwa inacheza dhidi ya Orlando Pirates.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli wakati Simba leo wakitarajiwa kuwa wenyeji wa Orlando Pirates katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza jijini Dar, Bumbuli alisema: “Nitafika Uwanja wa Mkapa Jumapili kwa ajili ya kuisapoti Simba, watani wetu ndiyo wawakilishi wa nchi pekee kwa sasa.

“Tunatamani kuona japo timu moja inachukua kikombe cha CAF ili timu za Tanzania ziwe zinaogopwa na kuheshimiwa. Tukienda nje hata wapinzani watuogope, hivyo watakuwa wakicheza kwa uoga.

“Hata wale Al Ahly, pale kwao Cairo, huwa wanazifunga baadhi ya timu kutokana na uoga.

Leo saa 1:00 Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Orlando mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Previous articleKIUNGO MGUMU KANOUTE PINI ZAKE ILIKUWA DK 419
Next articleMBADALA WA KANOUTE NA ONYANGO NI HAWA