KAZI INAANZA,KIMATAIFA, SIMBA YASHINDA BAO 1-0 ORLANDO PIRATES

Dakika 90 za kwanza zimekamilika kwa Simba kushinda bao 1-0 Orlando Pirates.

Ni asilimia 55 kwa Simba umiliki huku 45 ikiwa ni kwa Orlando Pirates.

Mtupiaji ni Shomari Kapombe kwa mkwaju wa penalti dk 65 na aliyesababisha penalti ni Bernard Morrison ambaye alikwama kumaliza dk 90 baada ya kuumia.

Timu zote mbili hakuna ambayo imeotea ndani ya dk 90 na Orlando Pirates walicheza mpira mkubwa kuanzia dk ya 70 mpaka 90 baada ya kufunguka kusaka ushindi.

Orlando Pirates walikuwa bora ndani ya dk 90 na kuweza kuzuia makali ya Simba katika Uwanja wa Mkapa hivyo kazi ni kubwa kwenda ugenini,Soweto.

Itakuwa ni Aprili 24,2022 na safari inaonekana kuwa ngumu zaidi kwa Simba kuweza kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuwa Orlando Pirates ni timu bora na imara.