Home International MWAMUZI WA KADI APEWA MANCHESTER CITY V LIVERPOOL

MWAMUZI WA KADI APEWA MANCHESTER CITY V LIVERPOOL

MICHAEL Oliver mwamuzi wa kati atakuwa kati leo kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA ambalo ni taji la pili kwa ukubwa kwa timu hizo kugombea kando ya ligi.

Itakuwa ni Uwanja wa Wembley saa 11:30 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ikiwa zimepita siku 7 tangu wababe hao wakutane Jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi na walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Mwamuzi huyua mwenye miaka 37 anasifika kuwa mwepesi kumwaga kadi kwa timu yoyote ile na mpaka sasa ametoa kadi 128 za njano na zile nyekundu 8.

Alikuwa mwamuzi wakati Manchester City ikishinda mabao 4-1 mbele ya Manchester United kwenye Manchester Derby Uwanja wa Etihad huku Liverpool wakishinda mabao 6-0 Leeds United Uwanja wa Anfield

Previous articleBIGIRIMANA WA RWANDA AINGIA ANGA ZA YANGA
Next articleEXCLUSIVE:HENRY JOSEPH AWAPA UJUMBE SIMBA