Home Sports BIGIRIMANA WA RWANDA AINGIA ANGA ZA YANGA

BIGIRIMANA WA RWANDA AINGIA ANGA ZA YANGA

BIGIRIMANA Obed kiungo wa Klabu ya Kiyovu ya Rwanda anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nai raia wa Tunisia.

Hesabu kubwa kwa sasa ndani ya vinara hao wa ligi msimu wa 2021/22 ni kuweza kusuka kikosi makini ambacho kitafanya vizuri kwenye mechi za kimataifa.

Kwenye msimamo Yanga ina pointi 51 ikiwa haijapoteza mchezo kati ya mechi 19 inapewa nafasi ya kuweza kutwaa ubingwa wa ligi kutokana na kasi ambayo wanakwenda nayo.

Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi wa Yanga wameonesha nia ya kuipata saini ya kiungo huyo hivyo ni suala la muda tu kuweza kukamilika usajili wa kiungo huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Injinia Hersi Said anatajwa kuwa mstari wa mbele kumfuatilia kiungo huyo ili aweze kusaini dili jipya ndani ya Yanga.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleMWAMUZI WA KADI APEWA MANCHESTER CITY V LIVERPOOL