Home Sports PRISONS YASHINDA BAADA YA SIKU 100

PRISONS YASHINDA BAADA YA SIKU 100

KLABU ya Tanzania Prisons ilikuwa kwenye kipindi cha mpito kwenye maisha yake ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na kushindwa kuvuna pointi tatu kwenye mechi ambazo walikuwa wanacheza.

Katika Ligi Kuu Bara ni timu ambayo ilikuwa kwenye nafasi ya 16 mpaka mzunguko wa kwanza ulipokamilika na sasa ni safari ya mzunguko wa pili umeanza.

Kwa sasa kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 19 ikiwa imeshinda mechi 4 na kulazimisha sare kwenye mechi 4.

Ilibidi iweze kusubiri kutimiza siku 100 kupata ushindi kwenye mechi za ligi. Mara ya mwisho kushinda ilikuwa Desemba 26,2021 Uwanja wa Kaitaba na ilishinda kwa bao moja baada ya hapo kwenye mechi 7 mfululizo haikuweza kushinda mpaka ilipotimia siku ya 100 waliposhinda mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Sokoine.

Tayari ilimpa mkono Shaban Kazumba ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo ambayo kwa sasa inatumia Uwanja wa Sokoine Mbeya na awali ilikuwa inatumia Uwanja wa Nelson Mandela.

Mabao hayo yalifungwa na Benjamin Asukile ambaye aliweza kufunga mabao hayo kwenye mchezo huo aliweza kupachika mabao hayo akitokea benchi na alipachika dk ya 77 na 90.


Previous articleBAYERN MUNICH IMEISHA,VILLARREAL YAISUBIRI LIVERPOOL/BENFICA
Next articleSAFARI NI NDEFU KUWEZA KUTOBOA KWENYE SOKA