Home International BAYERN MUNICH IMEISHA,VILLARREAL YAISUBIRI LIVERPOOL/BENFICA

BAYERN MUNICH IMEISHA,VILLARREAL YAISUBIRI LIVERPOOL/BENFICA

VIGOGO Bayern Munich hawataacha kulikumbuka jina la Samuel Chukwueze ambaye alipachika bao lililowafungashia virago katika mchezo wa hatua ya robo fainali.

Ni Robert Lewandowski mshambuliaji mahiri wa Bayern Munich alipachika bao la kuongoza dk ya 52 ila liliwekwa usawa zikiwa zimebaki dk 2 mpira kufika ukingoni.

Villarreal inasonga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa kuwa robo fainali ya kwanza ilikuwa ni sare ya kufungana bao 1-1.

Sasa Kocha Mkuu, Unai Emery wa Villarreal atakutana na Liverpool ama Benfica katika mchezo wa nusu fainali ya Champions League.

Liverpool inatarajiwa kumenyana na Benfica leo Aprili 13,Uwanja wa Anfield ambapo mchezo wa awali ubao ulisoma Benfica 1-3 Liverpool.

Previous articleBEKI WA ORLANDO PIRATES AKIMBIZWA HOSPITALI
Next articlePRISONS YASHINDA BAADA YA SIKU 100