SAFARI NI NDEFU KUWEZA KUTOBOA KWENYE SOKA

    DUNIA iliibatiza Afrika na nchi zake kuwa sehemu ya dunia ya tatu,ikiamini kuwa ni  dunia ambayo maisha ya mwanadamu wa kawaida yapo kwenye changamoto lukuki zinazofanya ndoto nyingi za vijana wa bara hili kuishia njiani au kutimiza kwa shida mno.

    Waafrika hupitia njia nyingi sana za shida, vikwazo vya kila aina katika kutimiza ndoto zao.

    Katika ramani ya soka vijana wengi Wakiafrika huathiriwa na changamoto hizi katika kutimiza ndoto zao na kuyafikia mafanikio, wengi wenye asili ya bara hili hupata ahueni ya safari hii pale tu wanapokuwa wamezaliwa na kukulia ng’ambo au la kuhamia wakiwa katika umri mdogo.

    Licha ya changamoto ya umaskini mkubwa na wakutupwa unaotesa familia nyingi za kiafrika, umaskini wa nchi uliozaa uhaba wa miundombinu, athari za kisiasa na vita za wenyewe kwa wenyewe pia zinazidi kupigilia msumari wa moto safari za utimizaji ndoto kwa vijana wengi wa bara hili.

    Hivi ushawahi sikia story ya Sadio Mane?, wakati Pierre Emerick Aubameyang akizaliwa na kukulia Spain, Sadio Mane amekulia huko kijijini katika mji wa Sedhiou nchini Senegal katika familia yenye rundo la umaskini.

    Stori ya Sadio Mane inabeba taswira halisi ya njia wanazopita nyota wengi Wakiafrika katika safari yao kisoka, kuanzia Mbeya,Mwanza,Ruvuma na miji mingine kama  Younde, Douala Cameron, Pwani ya Ivory, Gambia, Guinea, Angola mpaka kwetu Afrika ya Mashariki na Kusini.

    Safari za akina Yaya Toure na ndugu yake Kolo Toure zilijaa changamoto isiyoelezeka, vipi kuhusu wale watoto wa Accra?

    Ushawahi sikia stori ya Lamptey kuendesha baiskeli kutoka Ghana mpaka Nigeria kutafuta nafasi ya kutimiza ndoto zake kisoka?

    Ushawahi sikia stori za watoto wa Nigeria wanavyohangaika kule makoko kucheza soka? Huko ndiko akina Jay Jay Okocha, Taribo West na wengine wengi waliposotea ndoto zao, huko ndiko wale vijana walipoamua kudanganya umri ili mradi tu watimize ndoto zao.

    Ni changamoto hizo wanazopitia Waafrika katika kutimiza ndoto zao kisoka,wakati Harry Kane akianzia soka lake katika Academy toka akiwa na miaka 5,kijana Wakiafrika pale Goma nchini DRC anahangaika kuyaokoa maisha yake dhidi ya waasi wa msituni.

    Kijana mwingine anakimbiza uhai wake kule Mogadishu dhidi ya Al Shababi, soka wanalicheza kwenye ardhi yenye shida, milio ya risasi, mabomu, bila ya viatu huku mpira ukiwa haujulikani hata kampuni iliyoyengenezwa kwa kuchakaa kwake.

    Vuta picha zile purukushani alizokutana nazo mtoto wa Mbagala na shujaa Watanzania Mbwana Ally Sammata.

    Kucheza kwenye viwanja vyenye uzio wamabati yenye tishio la mbwa mkali, kisha kutembea kwa miguu kutoka Mbagala Zakhem mpaka Uwanja wa Mabatini ulioko Tandika kwenda kucheza mechi moja ya ndondo.

    Hii ndio Afrika na changamoto zake, ndiyo,tunafika lakini changamoto zake ni kubwa kuliko,haikupaswi uwe mzembe kuja kuyafikia mafanikio ya mpira,sio Tanzania pekee hii ni Afrika nzima.

    Previous articlePRISONS YASHINDA BAADA YA SIKU 100
    Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI