Home Sports SIMBA KAZINI LEO MBELE YA COASTAL UNION,MKWAKWANI

SIMBA KAZINI LEO MBELE YA COASTAL UNION,MKWAKWANI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba leo Aprili 7 anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.

Pablo amesema kuwa anadhani ni moja ya mchezo utakaokuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuhitaji kupata pointi tatu muhimu.

”Ninajua kwamba kila mmoja anahitaji kuona kwamba namna gani tunaweza kupata ushindi kwani jambo la msingi ni pointi tatu muhimu.

“Ambacho tunahitaji ni kuweza kucheza vizuri na kuongeza juhudi kwenye mechi ambazo tutacheza kwani wapinzani wetu tunakumbuka tulikutana nao mzunguko wa kwanza,”

Simba ilipokutana na Coastal Union, Uwanja wa Mkapa waligawana pointi mojamoja bila kufungana.

Coastal Union kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 18 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 37 bada ya kucheza mechi 17.

Previous articleYANGA YAICHAPA KWA MARA NYINGINE AZAM FC KWAO
Next articlePAMBANO LA DILLIAN WHYTE NA FURRY LIMEKUFA