Home Sports PAMBANO LA DILLIAN WHYTE NA FURRY LIMEKUFA

PAMBANO LA DILLIAN WHYTE NA FURRY LIMEKUFA

PAMBANO la bondia Dillian Whyte na Tyson Fury limekufa rasmi, Whyte hatocheza tena pambano lake la ubingwa wa dunia uzito wa juu dhidi ya Fury Aprili 23, mwaka huu, baada ya kupata jeraha la bega wakati akijiandaa na pambano hilo.

Mapromota wa pambano hilo, Frank Warren na Bob Arum, wamethibitisha kuwa, Fury ambaye ni bingwa wa WBC bado atapambana siku hiyo ya Aprili 23, Uwanja wa Wembley jijini London.

Mapromota hao walisema mashabiki 100,000 waliokata tiketi kushuhudia pambano la Whyte na Fury wana haki ya kushuhudia pambano usiku huo kwa kuwa wameshanunua tiketi.

Hivyo basi anatafutwa mpinzani mbadala wa Whyte, kutoka katika orodha ya mabondia 15 bora shindani wa WBC.

Ambapo mabondia watatu Joe Joyce, Agit Kabayel na Robeet Helenius wanatajwa kama mabondia walio mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Whyte.

Hii sio mara ya kwanza kwa Whyte kuumia bega na kuondolewa kwenye pambano, aliwahi kuumia bega na kuondolewa katika pambano dhidi ya Otto Wallin Oktoba mwaka jana.

Pia mwezi Desemba mwaka 2015 ilimlazimu kufanyiwa upasuaji wa bega baada ya pambano lake na Anthony Joshua.

Previous articleSIMBA KAZINI LEO MBELE YA COASTAL UNION,MKWAKWANI
Next articleCOURTOIS AANZA KUJISHTUKIA KUZOMEWA CHELSEA