Home Sports COURTOIS AANZA KUJISHTUKIA KUZOMEWA CHELSEA

COURTOIS AANZA KUJISHTUKIA KUZOMEWA CHELSEA

NI kama ameanza kujishtukia vile. Thibaut Courtois anatarajiwa kurudi kwenye uwanja wake wa zamani wa Stamford Bridge leo Jumatano katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kipa huyo Mbelgiji wa Real Madrid amesema: “Natumaini kwamba (mashabiki Chelsea) hawatanizomea.”

 

 

Real Madrid itatarajia kulipiza kisasi cha kufungwa katika nusu fainali ya michuano hiyo msimu uliopita, na hilo litategemea zaidi muendelezo wa kiwango bora kwa Courtois.

 

“Natumaini kwamba hawatanizomea, lakini huwezi kujua,” alisema Courtois.

 

“Nimejiandaa kwa chochote kitakachotokea. Natumaini itakuwa ni urejeo wa furaha Stamford Bridge. Sasa tumekuwa wapinzani. Watataka kushinda na hilo ndilo hata mimi nataka, kwa hiyo sitarajii kushangiliwa na mashabiki.”

Previous articlePAMBANO LA DILLIAN WHYTE NA FURRY LIMEKUFA
Next articleWAWEKEZAJI WAWEKEWE MAZINGIRA MAZURI, WAKIONDOKA ITAKUWA AIBU KWETU