PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ni pongezi kubwa wanastahili wachezaji,mashabiki pamoja na uongozi kwa kuweza kushuhudia timu hiyo ikipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya USGN na kuweza kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho usiku wa kuamkia leo Aprili 4,2022.
Pia Pablo amesema kuwa wapinzani wao walikuwa imara kwa kuwa hesabu zao ilikuwa ni kuweza kupata ushindi jambo ambalo liliwafanya wacheze kwa juhudi Uwanja wa Mkapa.