Home Sports YANGA YAIPIGIA HESABU AZAM FC

YANGA YAIPIGIA HESABU AZAM FC

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu muhimu.

Baada ya kucheza mechi 18 ni pointi 48 wamekusanya wakiwa nafasi ya kwanza wanatarajia kumenyana na Azam FC Jumatano ya Aprili 6,2022.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 28 baada ya kucheza mechi 18.

Kaze amesema;”Kwa sasa tunajua mchezo wetu ujao utakuwa dhidi ya Azam FC na hautakuwa mwepesi kutokana na wapinzani wetu nao kuwa bora na wanahitaji matokeo kwenye mchezo wetu.

“Jambo la msingi ni kufanya maandalizi mazuri kuanzia kwa wachezaji ambao wanajua kwamba tunahitaji pointi tatu, wapo wachezaji ambao tutawakosa ila tuna wachezaji wengine ambao wameanza kurudi kwenye ubora wao,” amesema.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 2-0 Azam FC.

Previous articleKIUNGO MGHANA ACHAGUA KUCHEZA NA FEISAL NA SURE
Next articleVIDEO:PABLO AWASHURUKU MASHABIKI USHINDI WA 4G KIMATAIFA