VURUGU kubwa ilitokea usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kati ya Nigeria dhidi ya Ghana.
Ubao wa Uwanja wa Moshood Abiola nchini Abuja ulisoma Nigeria 1-1 Ghana na Nigeria kuweza kufungashiwa virago kwa Ghana kupata faida ya bao la ugenini na jumla waliweza kufungana bao 1-1.
Baada ya mchezo huo kukamilika mashabiki wa Nigeria maarufu kama Super Eagles walikuwa na hasira kwa timu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia tena wakiwa nyumbani waliweza kushuka moja kwa moja eneo la uwanja.
Mashabiki hao walijaribu kuwashambulia wachezaji wa timu ya Taifa ya Ghana na kuharibu baadhi ya miundombinu ya uwanja na kuna video ambayo ilichukuliwa ikionyesha mabomu ya machozi ili kuweza kuwasambaratisha mashabiki hao waliokuwa na hasira kali.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ghana ilikuwa ni sare bila kufungana Uwanja Ohene Djan huko Kumasi na Super Eagels waliamini kwamba itakuwa ni rahisi kwa wao kuweza kufuzu jambo ambalo lilikuwa ni tofauti.
Ghana walianza kufunga kwenye mchezo huo dk ya 10 kupitia kwa Thomas Partey iliwapa nguvu ya kupambana huku lile la Nigeria likifungwa na nahodha wa Super Eagles William Troost-Ekong ilikuwa dk ya 22.
Ghana inakuwa ni timu ya kwanza kuweza kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia.