Home International WALIOITWA STARS WAFANYE KWELI,TUNAWAAMINI

WALIOITWA STARS WAFANYE KWELI,TUNAWAAMINI

TUMEONA tayari orodha ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa sasa imewekwa hadharani ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kimataifa zilizo kwenye Kalenda ya Fifa.

Hili ni jambo kubwa kwa wachezaji kuweza kujiona wakiwa wametajwa kwenye orodha kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Ni fahari na inapendeza ikiwa wale ambao wataitwa watatimiza majukumu kwa wakati bila kuweka zile sababu ambazo wakati mwingine zimekuwa zikiwafanya waweze kuondolewa kwenye kikosi kimyakimya.

Iliwahi kutokea hivi karibuni miongoni mwa wachezaji ambao waliitwa kwenye timu ya Taifa Stars walishindwa kuwasili ikiwa ni pamoja na Jonas Mkude na taarifa zikawa ni kwamba ana matatizo ya kifamilia lakini kwenye klabu alikuwa akiendelea na mazoezi.

Hii nina amini kwamba haitaweza kujirudia na kila aliyeweza kuitwa atakuwa katika furaha ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mechi ambazo atacheza.

Iwe ni mechi za kirafiki kwa kuwa ni za kimataifa hapo kuna jambo ambalo linapaswa lifanywe na kila mchezaji kuweza kuonyesha ule uwezo bila kuhofia.

Ukweli ni kwamba kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa hata zikiwa ni za kirafiki hiyo ni rekodi moja kali na itakuwa inaishi muda wote.

Pongezi kwa wale ambao wameweza kuitwa na wale ambao bado hawajaitwa haina maana kwamba wao sio bora hapana.

Kikubwa ni kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi za ndani na zile za kimataifa hilo litafanya mwalimu aweze kuona kile ambacho kipo kwa wachezaji wetu.

Tatizo kubwa limekuwa kwenye upande wa ushambuliaji hapa bado jitihada inahitajika huku kwa upande wa viungo kukiwa kuna angalau huku kwa mabeki unaweza kusema kwamba tunazidi kuimarika.

Basi ikawe ni kazi kubwa ya kusaka ushindi kwenye mechi zote ambazo tutakwenda kucheza na hilo litakuwa ni kwa ajili ya Tanzania yetu.

Wachezaji ikifika siku ya mechi jambo lenu liwe moja tu kusaka ushindi bila kuchoka na nina amini kwamba inawezekana.

Ushindi kwenye mechi yenu itaongeza hali ya viwango katika ubora kwani bado hatujawa imara katika hilo hapo ni muhimu kufanya vizuri.

Previous articleVIDEO:NAMNA YANGA WALIVYOTOA MSAADA OCEAN ROAD
Next articleKISA KUSHANGILIA LAMPARD AVUNJIKA,ALLAN ALIMWA NYEKUNDU