Home International LIVERPOOL YAICHAPA ARSENAL 2-0, YAISOGELEA MANCHESTER CITY

LIVERPOOL YAICHAPA ARSENAL 2-0, YAISOGELEA MANCHESTER CITY

VIJANA wa Jurgen Klopp wa Liverpool walizima ndoto za vijana wa Mikel Arteta wa Arsenal kuvuna pointi katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Emirates uliasoma Arsenal 0-2 Liverpool mbele ya mashabiki 59,968.

Diogo Jota kipindi cha pili dk 54 alijaza kimiani na bao la pili lilijazwa kimiani na Robert Firmino dk 62 ambaye alianzia benchi katika mchezo huo.

Arsenal walikuwa na nafasi ya kushinda kupitia kwa Martin Odegaard ambaye alishindwa kumtungua Alisson Becker ila haikuwa bahati kwake.

Ushindi huo unafanya Liverpool kufikisha pointi 69 tofauti ya pointi moja na vinara Manchester City ambao wana pointi 70 wote wakiwa wamecheza mechi 29.

Arsenal ipo nafasi ya 4 na pointi zake ni 51 baada ya kucheza mechi 27.

Previous articleVIDEO:CHAMA,BANGALA,AUCHO KUCHEZA MECHI MOJA JUNI
Next articleSIMBA KUKWEA PIA KUWAFUATA WAPINZANI WAO ASEC