Home Sports MSHAMBULIAJI WA SIMBA AKUBALI UWEZO WA MAYELE,AMPA TUZO

MSHAMBULIAJI WA SIMBA AKUBALI UWEZO WA MAYELE,AMPA TUZO

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ambaye hivi sasa anacheza Kagera Sugar, Mganda, Hamis Kiiza ‘Diego’amesema kuwa Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga ana uwezo mkubwa wa kucheza na kufunga.

Kiiza aliyewahi kuichezea Yanga kabla ya kwenda Simba, alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Februari 27,2022.

Yanga ilishinda mabao 3-0 yakifungwa na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’na Mayele aliyepachika mawili na kufikisha mabao 9.

Kiiza ametupia bao moja aliwafunga Simba katika mchezo wa ligi, amesema kuwa kwa aina ya uchezaji na mfumo ambao wanautumiaYanga, mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi msimu huu.

Nyota huyo amesema:“Kwa aina ya uchezaji na kimbinu wanayotumia wachezaji wenzake kumchezesha Mayele, basi namtabiria kufanya mengi mazuri katika msimu huu ikiwemo kutwaa ufungaji bora.

“Yanga mashambulizi yao wanayatumia kupitia pembeni kwa maana ya kupiga krosi ambazo zote wanampigia Mayele, ni kitu ambacho wanaonekana kukifanyia kazi mazoezini.

“Mabao yote aliyotufunga Mayele yametokea pembeni moja la krosi na lingine la faulo iliyotokea pembeni ambayo yote yakifungwa kwa kichwa,” amesema Kiiza.

Kibindoni ametupia mabao 9 Mayele akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Yanga huku mtupiaji namba moja akiwa ni Relliats Lusajo anayekipiga Namungo.

Previous articleABRAMOVICH ATHIBITISHA KUIWEKA SOKONI CHELSEA
Next articleTANZANIA PRISONS BADO WAPO PALEPALE