KOCHA CHELSEA ATAKA ALAUMIWE YEYE

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Thomas Tuchel ameweka wazi kuwa kipa wake Kepa Arrizabalaga hapaswi kulaumiwa kwa kukosa penati na hawezi kujutia kwa nini alimpa nafasi dakika za mwisho.

Katika fainali ya Carabao Cup iliyopigwa juzi Uwanja wa Wembeley, Kepa alikosa penati na kuipa nafasi Liverpool kutwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 11-10 ambazo alipata Chelsea.

Kwenye mchezo huo Edouard Mendy alianza langoni kwa upande wa Chelsea lakini ilipofika dakika 119 alitolewa na nafasi yake ilichukuliwa na Kepa.

“Nimefanya maamuzi kwa malengo mazuri ya kutaka kuwashinda wapinzani wetu ndiyo maana maamuzi yangu hayapaswi kujadiliwa.

“Ni kweli sijui nini kingetokea kama angekuwepo Eduo uwanjani ndio maana sitaki Kepa alaumiwe ni mimi ndiye ninayepaswa kulaumiwa,”.