SIMBA YAPOTEZA KIMATAIFA MBELE YA RS BERKANE

MAPAMBANO ambayo walikuwa wakifanya Simba mbele ya RS Berkane yamekwama kuwapa ushindi baada ya kupoteza kwenye mchezo wa kundi D kwa kufungwa mabao 2-0.

Adama Ba alipachika bao la kuongoza dakika ya 32 na lile la pili lilifungwa na Charki El Bahri dk 41 hawa waliimaliza Simba kipindi cha kwanza.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza Simba kupoteza kwenye mechi tatu ambazo wamecheza kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda mbele ya ASEC Mimosas kisha wakazimisha sare ya  kufungana bao 1-1 dhidi ya USGN ya Niger..

RS Berkane walipiga mashuti 19 na matano yaliweza kulenga lango huku mawili yakijaa nyavuni na kwa upande wa Simba ni mashuti mawili ambayo yalipigwa kwa Simba.

Mabao hayo yanaifanya Simba kuwa na pointi nne huku RS Berkane ikiwa nafasi ya kwanza na pointi ni 6 kwa RS Berkane huku Simba ikiwa na pointi 4.

Pablo Franco hakuwa na chaguo kwa wachezaji wake ambao kwenye eneo la ushambuliaji ilikuwa ni shida kupata nafasi kutokana na viungo kushindwa kutengeneza nafasi Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho wapo nafasi ya pili kwenye kundi D.