Home International PABLO AWEKA REKODI KIMATAIFA DAKIKA 180

PABLO AWEKA REKODI KIMATAIFA DAKIKA 180

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba ameweka rekodi yake kwenye mechi mbili mfululizo kuweza kufanya mabadiliko ambayo yamekuwa yakimpa matokeo ndani ya dakika 180.

Katika Kombe la Shirkisho mbali na kuwa Simba ni namba moja na pointi zake nne,pointi hizo zilipatikana kipindi cha pili mara baada ya kufanya mabadiliko kwa wachezaji ambao walikuwa benchi kuusoma mchezo.

Ilianza mbele ya ASEC Mimosas katika mchezo wa kwanza wa kundi D Simba kushuka uwanjani na ilikuwa ni Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda kwa mabao 3-1.

Ni mabao ya Pape Sakho aliyetupia kipindi cha kwanza huku Shomari Kapombe yeye alitupia kwa mkwaju wa penalti dakika ya 78 kwa penalti iliyosababishwa na Yusupph Mhilu ambaye alitoka benchi aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Sadio Kanoute na bao la tatu lilifungwa na Peter Banda kwa pasi ya John Bocco ambaye aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Meddie Kagere.

Juzi wakati Simba ikipata pointi moja mbele ya USGN ya Niger ni Bernard Morrison alitupia bao hilo yeye aliingia akitokea benchi dakika ya 64 alichukua nafasi ya Yusuph Mhilu.

Usiku wa jana Februari 21 kikosi cha Sima kilikuwa Uturuki na leo kinatarajiwa kuwasili Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya RS Berkane unaotarajiwa kuchezwa Februari 27.

Previous articleVIDEO;NYOTA WA YANGA SAINI YAKE ILIKUWA INAHITAJIKA SIMBA
Next articleVIDEO;ZAHERA AWAPA ONYO YANGA,AMTAJA ATAKAYEFUNGA HAT TRICK