>

FT:SIMBA 6-0 DAR CITY,KOMBE LA SHIRIKISHO

USHINDI wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City unaipa nafasi Simba kutinga hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho.

Ni katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na Simba waliweza kwenda mapumziko wakiwa wametupia mabao manne.

Ni Meddie Kagere alitupia mabao mawili huku Clatous Chama na Rally Bwalya wakitupia bao mojamoja.

Kipindi cha pili Pascal Wawa na Chris Mugalu hawa wote walitupia bao mojamoja na kufanya ubao wa Mkapa Simba 6-0 Dar City.

Simba ni mabingwa watetezi walitwaa mbele ya Yanga Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.