Home Sports YANGA WAMEPANIA, GSM WAMUITA MAYELE

YANGA WAMEPANIA, GSM WAMUITA MAYELE

YANGA kweli safari hii imepania kuhakikisha kuwa inawalinda mastaa wake hiyo ni baada ya uongozi wa klabu hiyo chini ya wadhamini wao, GSM kumuita fasta mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Fiston Mayele kwa ajili ya mazungumzo.


Fiston Mayele ndani ya Yanga
kwa sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao akiwa na jumla ya mabao 6 huku akiwa wapili kwenye orodha ya wafungaji bora. Kinara wa jumla ni Reliants Lusajo wa Namungo mwenye 7.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa, uongozi wa GSM umefanya
kikao na
Mayele ambaye amekuwa ni msaada wa timu na hiyo ni katika kuhakikisha kuwa anaendelea kusalia ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.


“Ni kweli Mayele leo
Jumanne (jana) alikutana na uongozi wa GSM ambao walikuwa na kikao na kubwa zaidi lilikuwa ni kuzungumza ni kwa namna gani mshambuliaji huyo anaendelea kusalia ndani ya timu kwa muda
mrefu licha ya kuwa tayari ana
mkataba wa miaka miwili ambao alisaini wakati anajiunga na timu hiyo.

“Unajua kuna mambo mengi kwenye mpira, unapokuwa na wachezaji wazuri lazima ufahamu jinsi ya kuishi nao na ndio maana vitu kama hivi uongozi kukaa kufanya vikao na mchezaji ni kawaida kwa ajili ya manufaa ya
pande zote mbili yaani mchezaji na
timu,” kilisema chanzo hiko.

Alipotafuta Mayele kuzungumzia juu ya ishu hiyo alisema: “Ni kweli nilikuwa na kikao na uongozi jambo
ambalo sio geni kwa wachezaji na
yalikuwa ni mambo binafsi ambayo nisingependa kuyaweka hadharani.”

Previous articleMASTAA YANGA WAKOMBA MABILIONI YA BONASI
Next articleWATATU WASHINDA TIKETI ZA AFCON NA CRDB