Home Sports WATATU WASHINDA TIKETI ZA AFCON NA CRDB

WATATU WASHINDA TIKETI ZA AFCON NA CRDB

MKURUGENZI wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kushoto) leo Januari 27,2022 amekabidhi mfano wa tiketi ya kushuhudia mechi ya fainali ya Mashindano ya AFCON nchini Cameroon kwa washindi watatu.

Hao ni wa washindi wa droo ya shinda na TemboCard Viza, ikiwa ni pamoja na Njama Ayoub Matumbo,Mwizegwa Osmond Rusibamayila na Ahmed Mohamed Baghozaha.

Katika hafla ya kukabidhi tiketi hizo kwa washindi wa mwezi Desemba 2021, iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam washindi walikuwa na furaha kuweza kuibuka na ushindi.

Washindi hao watashuhudia mubashara fainali za Kombe la Afcon ambalo bingwa mpya atapatikana nchini Cameroon.

Tayari bingwa wa Afcon ambaye alikuwa anapewa nafasi ya kufanya vizuri Algeria ambaye alishinda mbele ya Senegal katika fainali safari yake ilishaishia njiani hivyo atamtazama bingwa mpya kwa kideo.

Previous articleYANGA WAMEPANIA, GSM WAMUITA MAYELE
Next articleMABINGWA WATETEZI WAREJEA DAR